Abati (pia "abate") ni cheo cha mkuu wa monasteri yenye wamonaki wengiwengi (kwa kawaida 12 na zaidi) hasa katika Kanisa Katoliki.
Jina linatokana na Kilatini abbas, mkoko kutoka Kiaramu אבא (Abba, yaani "baba"). Kiongozi wa monasteri ya kike anaitwa pengine abesi.
Nchini Tanzania Wabenedikto wana maabati katima monasteri za Peramiho, Ndanda, Hanga na Mvimwa.
Maabati wachache wanapewa daraja takatifu ya askofu kwa kuwa monasteri yao ina jukumu la uchungaji kwa waamini wa eneo fulani (abasia ya kijimbo), kama ilivyokuwa kwa wale wa Peramiho na Ndanda wakati wa umisionari.