Abdon

Abdon (kwa Kiebrania עַבְדּוֹן, ‘Aḇdōn, "Mtumishi" au "Utumishi") alikuwa mmojawapo kati ya Waamuzi wa Biblia.

Kadiri ya Waamuzi 12:13-15 alikuwa wa kabila la Efraimu akaongoza Israeli kwa miaka 8[1].

Alikuwa na watoto wa kiume 40 na wajukuu wa kiume 30, ambao kila mmoja alikuwa na punda wake. Hii inaonyesha alikuwa tajiri.

  1. "The "Minor Judges"- A Re-evaluation". Alan J. Hauser. 1975. Iliwekwa mnamo 2015-03-27. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne