Abeli

Sanamu ya marumaru kwenye Kanisa kuu la Milano inayoonyesha Kaini alivyomuua Abeli.
Kaini akimuua Abeli, kadiri ya mchoro mdogo wa karne XV.

Abeli au Habili ni jina la mtu anayetajwa na Biblia kama mwana wa pili wa Adamu na Eva na kama binadamu wa kwanza kufa, akiwa ameuawa na kaka yake Kaini kwa kijicho.

Habari hizo zinapatikana katika kitabu cha Mwanzo (4:2-8), lakini Abeli alitajwa pia na Yesu kama mfiadini wa kwanza (Math 23:35).

Kurani inasimulia habari hiyo bila kumtaja Abeli (5:27-31).


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne