Abimeleki (kwa Kiebrania אֲבִימָלֶךְ, ’Ǎḇîmeleḵ[1]) mwana wa Gideoni [2] alikuwa mfalme wa Shekemu kwa muda mfupi wakati wa Waamuzi wa Biblia[3].
Kadiri ya Waamuzi 9:1-5 alipata ufalme kwa kuua ndugu zake wote 70, isipokuwa Yothamu aliyenusurika. Huyo alitoa hotuba yenye mfano dhidi ya Abimeleki na watu wa Shekemu waliomuunga mkono (Waamuzi 9:7-15).
Baada ya vita mbalimbali, alijeruhiwa vibaya na mwanamke aliyemrushia kutoka juu jiwe kubwa kichwani. Hapo aliagiza msaidizi wake ammalize kwa upanga.
Waamuzi 12 na wengineo |
---|