Abraham Lincoln | |
![]() | |
Muda wa Utawala Machi 4, 1861 – Aprili 15, 1865 | |
Makamu wa Rais | Hannibal Hamlin (1861–1865) Andrew Johnson (Machi–Apr. 1865) |
mtangulizi | James Buchanan |
aliyemfuata | Andrew Johnson |
tarehe ya kuzaliwa | Kentucky, Marekani | Februari 12, 1809
tarehe ya kufa | 15 Aprili 1865 (umri 56) Washington, D.C., Marekani |
mahali pa kuzikiwa | Lincoln Tomb |
chama | Whig (Kabla ya 1854) Republican (1854–1864) National Union (1864–1865) |
ndoa | Mary Todd Lincoln (m. 1842) |
watoto | Robert Todd Lincoln Edward Baker Lincoln William Wallace Lincoln Tad Lincoln |
signature | ![]() |
Abraham Lincoln (12 Februari 1809 – 15 Aprili 1865) alikuwa Rais wa 16 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1861 hadi 1865.
Alikuwa na Kaimu Rais wawili: kwanza Hannibal Hamlin, halafu Andrew Johnson aliyemfuata kama Rais, Lincoln alipouawa.
Lincoln amejulikana kama rais wa upande wa kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani kati ya majimbo ya kaskazini dhidi ya Shirikisho la Madola ya Amerika la kusini.
Kwa hiyo hukumbukwa kama rais aliyeleta mwisho wa utumwa, yaani uhuru kwa watumwa wote wa Marekani na kuunganisha taifa tena.
Juhudi zake zilimgharimu uhai.