Abrahamu au Ibrahimu na awali Abram (kwa Kiebrania: אַבְרָהָם He-Avraham, Avraham, ʼAḇrāhām, Avrohom au Avruhom, kwa Kiarabu إبراهيم Ibrahim; aliishi Mashariki ya Kati mwaka 1800 hivi K.K.) huheshimiwa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu kama mtakatifu, kielelezo cha mtu wa imani, rafiki wa Mungu.
Alipoitwa naye, alihama nchi yake, Iraq ya leo, akielekea nchi aliyoahidiwa kwa ajili yake na ya wazao wake.
Alitokeza imani yake yote kwa Mwenyezi Mungu pale ambapo, kwa tumainia yasiyotumainika, hakukataa kumtolea sadaka mwanae pekee Isaka, aliyepewa uzeeni kupitia mke tasa [1].