Adamu mpya

Utukufu wa mtoto Kristo mbele ya Mungu Baba na Roho Mtakatifu. Sehemu ya mchoro wa Daniel Gran Vienna, Austria. Adamu na Eva wamechorwa chini wamefungwa minyororo.
Yesu akiwatoa Adamu na Eva nje ya makaburi yao siku ya kiyama, Istanbul, Uturuki.

Adamu mpya, Adamu wa pili au Adamu wa mwisho (1Kor 15:45) ni kati ya majina ya Yesu katika Agano Jipya.[1][2][3]

Humo mara mbili Mtume Paulo anafananisha Yesu na Adamu.

Katika 1Kor 15:22 anasema, "kama vile katika Adamu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai" na katika mstari wa 45 unamuita Yesu "Adamu wa mwisho".

Halafu katika Rom 5:12–21 anasema, "kama vile kwa kosa la mtu mmoja wengi wamefanywa wakosefu, vivyo hivyo kwa utiifu wa mmoja wengi watafanywa waadilifu" (Rom 5:19).

  1. Watson E. Mills, Roger Aubrey Bullard, eds, Mercer dictionary of the Bible. 1998, p. 10. ISBN 0-86554-373-9
  2. James D. G. Dunn, The Theology of Paul the Apostle. 2006, p. 241 [1]. ISBN 0802844235
  3. John MacArthur, Matthew 1–7, Volume 1. 1985, p. 132. ISBN 0802407552

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne