Adiuto wa Cava

Sanamu yake.

Adiuto wa Cava (alifariki karne ya 5) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kusini lakini alikuwa mzaliwa wa Afrika Kaskazini.

Baada ya kuteswa na Wavandali Waario kwa sababu ya imani yake, alifukuzwa akiwa na wenzake 12, wakiachwa baharini katika meli mbovu isiyoweza kuendeshwa.

Labda wakati huo alikuwa askofu tayari. Baada ya kufika Italia aliongoza jimbo la Cava dei Tirreni.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne