Afrika hapo awali lilikuwa jina la jimbo la Dola la Roma katika mwambao wa Mediteranea huko Afrika Kaskazini miaka 146 KK - 698 BK. Eneo lake lilikuwa takriban Tunisia ya kaskazini pamoja na pwani ya Libya ya magharibi na Algeria ya mashariki.
Jimbo lilikuwa maarufu kama "ghala ya ngano" ya Roma.
Watu wa Afrika ya Kaskazini kiasili walikuwa hasa Waberber.
Miji muhimu ilikuwa Karthago na Leptis Magna.
Bara la Afrika limepokea jina lake kutoka jimbo hili. Waarabu waliendelea kutawala eneo lake kwa jina la jimbo la Ifriqiya ambalo ni matamshi yao ya "Afrika".