| |||
Mwanzo wa utawala wa kikoloni | 1885 | ||
Makao ya serikali ya kikoloni | Bagamoyo hadi 1891 halafu Dar es Salaam | ||
Eneo | km² 995,000 | ||
Wakazi | 7,665,234 (1-1-1913) | ||
Wakazi Wajerumani | 4,100 (1913) | ||
Pesa | 1 Rupie= 64 Pesa, kuanzia 1904 1 Rupie = 100 Heller | ||
Nchi huru za leo | 1961 Tanganyika, tangu 1964 Tanzania |
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (au: ya Kidachi; kwa Kijerumani Deutsch-Ostafrika -DOA-; kwa Kiingereza German East Africa) ilikuwa jina la koloni la Ujerumani huko Afrika ya Mashariki kati ya miaka 1885 na 1918/1919.
Eneo lake lilijumlisha nchi za kisasa za Tanzania bara (yaani bila Zanzibar), Burundi na Rwanda. Ilikuwa koloni kubwa kabisa la Dola la Ujerumani.