Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu mapendo |
![]() Moyo katika mapokeo ya Ulaya ni mchoro unaowakilisha mapendo. |
Vipengele Msingi |
---|
Mapendo kadiri ya sayansi |
Mapendo kadiri ya utamaduni |
Upendo (fadhila) |
Upendo safi |
Kihistoria |
Mapendo ya kiuchumba |
Mapendo ya kidini |
Aina za hisia |
Mapendo ya kiashiki |
Mapendo ya kitaamuli |
Mapendo ya kifamilia |
Mapendo ya kimahaba |
Tazama pia |
Mafungamano ya binadamu |
Jinsia |
Tendo la ndoa |
Maradhi ya zinaa |
Siku ya wapendanao |
Agape ni neno la lugha ya Kigiriki (ἀγάπη, agape) lenye maana ya "upendo". Ni muhimu hasa katika maandiko ya Agano Jipya na maandiko mengine ya Ukristo, unaojitambulisha kama dini ya upendo.
Kigiriki kina maneno mbalimbali kwa jambo linaloitwa "upendo" katika lugha mbalimbali ambazo zina neno moja tu. Kwa hiyo "agape" inataja maana ya pekee ya "upendo" ambayo ni upendo wa kindugu au upendo wa Mungu. Upande mwingine wa upendo kwa Kigiriki ni "philia" (undugu, pendo lisilo la kingono) na mwingine ni "eros" ambayo ni mapenzi yenye tabia ya kingono.
Agape ni aina ya upendo isiyotafuta faida wala tamaa wala ridhaa.
Katika maandiko ya Kikristo agape inamaanisha:
Chanzo kwa Wakristo ni amri (kiasili ya Agano la Kale) jinsi inavyopatikana kwa mfano katika Luka 10:27:
"Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe"
Wakati mwingine namna ya pekee ya kuadhimisha Chakula cha Bwana huitwa "agape".