Agrikola wa Avignon

Mt. Agrikola katika dirisha la kioo cha rangi la kanisa lake huko Avignon.

Agrikola wa Avignon (pia: Agricol, Agricola, Agricolus; 630 hivi - 700 hivi) alikuwa askofu wa 11 wa Avignon, Provence (leo nchini Ufaransa) tangu mwaka 660 hadi kifo chake.

Kisha kuishi kama mmonaki huko Lerins tangu umri wa miaka 16 hadi 30, alikwenda kumsaidia baba yake, Magnus, askofu wa Avignon, akawa mwandamizi wake[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Septemba[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/68680
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne