Aibati, O.S.B. (Espain[1], leo nchini Ubelgiji, 1060 hivi - karibu na Crespin, Hainault, leo nchini Ufaransa, 7 Aprili 1140) alikuwa mkaapweke, halafu mmonaki na padri[2] wa shirika la Mt. Benedikto[3].
Kila siku alikuwa akisali Zaburi zote akiwa amepiga magoti au kujilaza kifudifudi. Pamoja na hayo, alikuwa anawapatia huruma ya Mungu umati wa watu waliomtembelea[4].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[5].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[6].