Ali Kiba

Ali Kiba

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Ali Salehe Kiba
Amezaliwa Novemba 29 1986 (1986-11-29) (umri 38)
Asili yake Iringa, Bendera ya Tanzania Tanzania
Aina ya muziki Mwanamuziki
Kazi yake Mwimbaji Mwanasoka
Aina ya sauti Sauti, piano
Miaka ya kazi 2006 hadi sasa
Studio Rockstars4000
Kings Music
Ame/Wameshirikiana na Aslay
Abdu Kiba
Christian Bella
Ommy Dimpoz
M.I
Patoranking
Abby Skills
Mr. Blue

Ali Kiba (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ali Salehe Kiba; pia: King Kiba; alizaliwa mkoani Iringa, 26 Novemba 1986) ni mwanamuziki wa Tanzania, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo chini ya lebo yake ya King's Music records na lebo aliyokuwa akiifanyia kazi Rockstar4000, ambayo alikuwa miongoni mwa wamiliki wake.

Ana vipaji vilivyo tofauti na wasanii wenzake, hivyo amejikita sehemu nyingine kwa kusajiliwa na timu ya mpira wa miguu "Tanga Coastal Union" ya mkoani Tanga kucheza mpira wa miguu kwa msimu wa 2018/2019 wa Vodacom Premier League. Lakini pia Ali kiba ni mmiliki wa media ya habari ya Crown mediailiyopo na makazi yake jijini Dar es Salaam.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne