Ali Hassan Mwinyi | |
![]() | |
Muda wa Utawala 5 November 1985 – 23 November 1995 | |
Waziri Mkuu | Joseph Sinde Warioba |
---|---|
mtangulizi | Julius Nyerere |
aliyemfuata | Benjamin Mkapa |
tarehe ya kuzaliwa | 8 Mei 1925 Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
ndoa | Siti Mwinyi |
dini | Uislamu |
Ali Hassan Mwinyi (8 Mei 1925 - 29 Februari 2024) alikuwa Rais wa pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 1990 hadi 1996.
Kabla ya hapo alikuwa Rais wa tatu wa Zanzibar baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Aboud Jumbe Mwinyi kwenye Januari 1984. Urais wa Zanzibar ulimfanya kuwa makamu wa rais wa Tanzania; hivyo aliteuliwa kugombea urais wa kitaifa wakati Julius Nyerere alipoamua kutogombea tena kwenye mwaka 1985. Mwinyi alichaguliwa akaacha cheo chake cha Zanzibar akawa rais wa Tanzania. Visiwani alifuatwa na Idris Abdul Wakil.
Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais.