Ali Larter | |
---|---|
![]() Larter at the 64th Annual Golden Globe Awards. | |
Amezaliwa | Alison Elizabeth Larter 28 Februari 1976 Cherry Hill, New Jersey, U.S. |
Jina lingine | Allegra Coleman[1] |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1997–hadi sasa |
Ndoa | Hayes MacArthur (2009–hadi sasa) |
Alison Elizabeth "Ali" Larter (amezaliwa tar. 28 Februari 1976) ni mwigizaji wa fiamu na mwanamitindo wa zamani kutoka nchini Marekani. Ameanza kazi za uigizaji ni baada ya kuonekana kidogokidogo kwenye vipipindi kadhaa vya televisheni kunako miaka ya 1990. Kuanzia 2006 hadi 2010, Larter amecheza nyusika za Niki Sanders halafu ndugu wa kashinde wake-waliopoteana muda mrefu Tracy Strauss kwenye mfululizo wa TV wa ubunifu wa kisayansi wa kwenye NBC, Heroes.[2][3]
Larter ameanza kazi kama mwanamitindo lakini baada ya muda mfupi akajiingiza kwenye masuala ya uigizaji. Ameanza kujipatia umaarufu wa hali ya juu baada ya kushiriki kwenye filamu ya mwaka wa 1999, Varsity Blues. Hii ilifuatiwa na filamu ya kutisha ya House on Haunted Hill (1999), Final Destination (2000), na Legally Blonde (2001). Tangu hapo, akaanza kucheza kwenye nyusika za juu tena ikiwa ni pamoja na kurudia uhusika wake kwenye Final Destination 2 (2003), amecheza kama muhusika wa jina tu kwenye filamu ya Bollywood ya Marigold (2007) na kucheza kama muhusika wa mchezo wa video Claire Redfield kwenye Resident Evil: Extinction. Hivi karibuni, amecheza kwenye picha ya kusisimua ya mwaka wa 2009, Obsessed.
Larter amepewa jina kwenye orodha ya "Wanawake Wazuri Walio-Hai".[4] Ameolewa na bwana wake aliyedumu naye kwa muda wa miaka mitatu, Hayes MacArthur, kwa sherehe ndogo tu huko mjini Maine mnamo tar. 1 Agosti 2009.[5]
{{cite web}}
: Check date values in: |accessdate=
(help)