Amanda Palmer (mwandishi habari)

Amanda Palmer (alizaliwa 1976) anaongoza uzinduzi wa Doha Tribeca Film Festival (DTFF) na ni Mkuu wa Burudani wa Al Jazeera ya Kiingereza.

Amanda Palmer

Palmer alijiunga na DTFF kutoka Al Jazeera ya Kiingereza, ambapo kama Mkuu wa Burudani anaunda, na kutayarishwa, vipindi vya elimu na sanaa katika mtandao wa Al Jazeera. Kipindi chake cha "48" kilichochaguliwa kupata tuzo na kipindi cha "The Fabulous Picture Show," (FPS) kinachojulikana kote duniani vimemfanya ajulikane kama mtaalam wa utamaduni.

Kazi ya Palmer imesababisha watengezaji filamu wajulikane kote duniani. Kwa kujenga jukwaa la kimataifa la watengezaji filamu, Palmer amegundua talanta mpya na zinazoibukia ambayo imesababisha idadi ya wasanii wengi kupata fursa ya kuzungusha filamu zao. Katika kazi yake kwa jumla, Palmer hajawahi kusita kueleza changamoto anazopata ikiwa anarikodiwa kwa kamera au hata kazi yoyote nyingine isiyohitajiwa kurikodiwa. Baada ya kupokea shahada yake ya sanaa katika uandishi habari kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia mjini Sydney, Palmer alisomea maonyesho na muziki. Alianza kazi kama mwandishi habari wa kitaifa kwa mtandao wa Channel Seven nchini Australia kabla ya kuhamia jijini London na kuwa mwanamke mdogo zaidi kuwahi kufanya kazi kwenye stesheni iliyo Ulaya. Yeye kisha alihamia CNN na baadaye Associated Press TV kabla ya kujiunga na Al Jazeera ya Kiingereza mnamo Agosti 2005. Sasa yeye yumo katika Kamati cha Filamu Nchini Qatar.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne