Amato wa Sion (pia: Amat, Amé, Aimé; alifariki Breuil-sur-le-Lys, karibu na Amiens, Ufaransa, 690 hivi) alikuwa mmonaki Mkolumbani, halafu askofu wa mji huo, leo nchini Uswisi kuanzia mwaka 669, lakini baada ya miaka 5 ya uongozi bora alipelekwa uhamishoni na mfalme Theodoriki III[1] akafariki huko [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Septemba[3].