American Association of People with Disabilities

American Association of People with Disabilities (kifupi: AAPD; yaani Chama cha Watu wenye Ulemavu Marekani) ni shirika la Marekani lisilo na faida, ambalo hutetea haki za kisheria za watu wenye ulemavu, lenye makao makuu yake mjini Washington, D.C.[1]

Dhamira ya AAPD ni kuongeza nguvu ya kisiasa na kiuchumi kwa watu wenye ulemavu. Kama shirika la haki la Kitaifa linaloongozwa na watu wenye ulemavu mtambuka, AAPD inatetea haki za kiraia kikamilifu, ambapo ni zaidi ya Wamarekani millioni 60 wenye ulemavu. AAPD inahimiza fursa sawa; kiuchumi, uhuru wa kuishi na ushiriki kisiasa kwa watu wenye ulemavu.[2]

Moja ya malengo ya msingi ya AAPD ni kuhimiza zaidi utekelezaji wa Sheria ya Wamarekani wenye ulemavu.[1]

  1. 1.0 1.1 "Home". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.
  2. "About". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne