Anastasi wa Aleksandria (alifariki 18 Desemba 616) alikuwa patriarki wa 36 wa Kanisa la Kikopti kuanzia mwaka 605 hadi kifo chake, kipindi cha dhuluma kubwa dhidi ya Wakopti.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].