Andorra

Principat d'Andorra
Utemi wa Andorra
Bendera ya Andorra Nembo ya Andorra
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Virtus Unita Fortior
(Kilatini: "Tabia nzuri ya pamoja ina nguvu zaidi")
Wimbo wa taifa: El Gran Carlemany, Mon Pare
(Kikatalani: "Karolo Mkuu baba yangu"
Lokeshen ya Andorra
Mji mkuu Andorra la Vella
42°30′ N 1°31′ E
Mji mkubwa nchini Andorra la Vella
Lugha rasmi Kikatalani
Serikali Bunge - Utemi wa pamoja
{{{leader_names}}}
Uhuru
Paréage
1278
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
468 km² (ya 193)
--
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2004 sensa
 - Msongamano wa watu
 
67,313 (ya 202)
69,150
152/km² (ya 69)
Fedha Euro (€) (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .ad[1]
Kodi ya simu +376

-


Ramani ya Andorra

Utemi wa Andorra (Kikatalani: Principat d'Andorra, Kifaransa: Principauté d'Andorre) ni nchi ndogo katika Ulaya ya kusini magharibi.

Katiba yake ni ya utemi lakini kuna watemi wawili, nao wako nje ya nchi. Mmoja ni rais wa Ufaransa na mwingine ni askofu wa Urgell katika Hispania.

Andorra ni nchi mwanachama ya Baraza la Ulaya lakini si ya Umoja wa Ulaya. Hivyo si sehemu ya eneo la kodi za pamoja la Ulaya. Hali hii inavuta watalii kwa sababu bidhaa nyingi zinapatikana bila kodi kwa bei nafuu kuliko Hispania au Ufaransa; kodi ya ongezeko la thamani (VAT) iko kwenye 4% pekee.

Andorra inatumia pesa ya Euro bila kushiriki katika mkataba wa Euro.

Siku hizi imekuwa nchi tajiri kutokana na utalii.

  1. .cat shared with Catalan-speaking territories.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne