Android

Android ni jina la aina ya mfumo huria wa uendeshaji wa simu za mikononi. Mfumo huo hutumiwa hasa katika simujanja, kama vile Google inavyomiliki Google Nexus, vilevile kampuni nyingine zinafanya vivyohivyo ikiwa ni pamoja na HTC na Samsung. Mfumo huo wa uendeshaji umepata kutumika pia katika kompyuta bapa kama vile Motorola, Xoom na Amazon Kindle Fire. [1]

Google imetoa pia Android nyingine kama vile Android TV ya televisheni, Android Auto ya magari, Android Things kwa ajili ya vifaajanja na Wear Os ya saa ya mkononi. Aina nyingine za Android hutumiwa pia kwa michezo ya kompyuta na kamera za kidijiti.

Android mwanzoni iliundwa na Android Inc. kabla ya kununuliwa na Google mwaka 2005. Matumizi rasmi ya kibiashara yalianza mnamo Septemba 2008. Toka mwaka huo Android imetoa matoleo mbalimbali. Toleo la sasa ni 9 "Pie" lililotolewa Agosti 2018. Android Q beta ilitolewa Machi 13, 2019. Programu ya msingi ya Android inaitwa Android Open Source Project (AOSP) ambayo hutolewa kwa Leseni ya Apache.

Google inasema zaidi ya simujanja milioni 1.3 zenye mfumo wa Android zinauzwa kila siku.[2] Hii imeifanya Android kuwa miongoni mwa mifumo ya uendeshaji wa simu inayotumika sana duniani.

  1. Android Project Home
  2. "There Are Now 1.3 Million Android Device Activations Per Day". TechCrunch. 2012-09-05.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne