Anna Line (1563 hivi – 27 Februari 1601) alikuwa mwanamke Mwingereza aliyebadilisha imani yake ya dini kutoka Ushirika wa Anglikana kuingia Kanisa Katoliki.
Kwa vile aliwaficha mapadri nyumbani mwake na kuhudhuria Misa zao, alipelekwa mahakamani na kuuawa kwa kunyongwa[1].
Mwaka 1929 alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenyeheri na mwaka 1970 alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini.