Ansberto wa Rouen (pia: Auedebati, Autbati, Autbertus; Chaussy-sur-Epte, leo nchini Ufaransa, karne ya 7 – Hautmont, 695 hivi) alikuwa askofu wa Rouen (Ufaransa) miaka 683 - 690.
Baada ya kushika vyeo vikubwa katika ikulu alijiunga na monasteri chini ya kanuni ya Kolumbani na miaka sita baadaye akawa abati. Hatimaye alifanywa askofu hadi alipoondolewa na Meya wa ikulu akarudia maisha ya monasterini[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Februari.[2]