Ansfridi

Sanamu ya Mt. Ansfridi huko Huy.

Ansfridi (Ubelgiji, 940 hivi – Leusden, leo nchini Uholanzi, 3 Mei 1010) alikuwa mtawala wa Huy, maarufu kwa maadili ya Kikristo pamoja na mke wake na binti yao pekee.

Alipofiwa mke wake, alitaka kujiunga na monasteri, lakini kaisari Oto III alimfanya askofu mkuu wa Utrecht mwaka 955 akaongoza jimbo hilo hadi kifo chake, ingawa alipozidi kudhoofika kutokana na malipizi yake akawa mmonaki kama alivyotamani kama moja ya monasteri alizozianzisha [1][2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe 3 Mei[3].

  1. Butler, Alban and Burns, Paul. Butler's Lives of the Saints, Vol. 5, A&C Black, 1997 ISBN 9780860122548
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/51740
  3. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne