Asali ni chakula kitamu katika hali kiowevu kinachotengenezwa na nyuki.
Nyuki hula mbelewele pamoja na maji matamu ndani ya maua na kuitoa tena katika mzinga wa nyuki kwa kuitunza kwenye sega. Ndani ya sega kiowevu huiva kuwa asali kamili.
Asali inavunwa na watu na kuwa chakula muhimu. Asali hujenga afya. Katika nchi za kaskazini ilikuwa njia ya pekee ya kutia utamu kwenye chakula kabla ya kupatikana kwa sukari kwa njia ya biashara ya kimataifa.