Ashuru (ebr. אַשּׁוּר ) ni jina la mtu katika kitabu cha Mwanzo cha Biblia.
Kufuatana na masimulizi ya Mwanzo 10:11 alikuwa mwana wa pili wa Shemu mwana wa Nuhu. Kaka zake waliitwa Elamu, Arfaksadi, Ludi na Aramu[1].
Hakuna taarifa katika Biblia kuhusu ukoo wa Ashuru.
Ashuru ni pia jina la mji wa Ashuru na milki ya Ashuru na maeneo yao.
Katika Mwa. 10:11 haieleweki vizuri kama jina "Ashuru" linamtaja mtu au mji[2]. Matoleo ya Biblia kwa lugha mbalimbali zinatafsiri tofauti hapa.