Jiji la Aswan | |
Mahali pa mji wa Aswan katika Misri |
|
Majiranukta: 24°05′20″N 32°53′59″E / 24.08889°N 32.89972°E | |
Nchi | Misri |
---|---|
Mkoa | Aswan |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 275,000 |
Tovuti: www.aswan.gov.eg |
Aswan (kwa Kiarabu أسوان, Aswān, pia Assuan au Assouan) ni mji wa kusini kabisa nchini Misri wenye wakazi 200,000. Ni makao makuu ya mkoa wa Aswan. Imejulikana duniani kutokana na lambo la Aswan ambalo ni ukuta mkubwa unaozuia mwendo wa mto Nile na kusababisha kutokea kwa bwawa la Nasser.
Tangu kutengenezwa kwa lambo hilo, Aswan imekuwa mji wa viwanda kwa sababu umeme unapatikana kwa wingi tangu 1960.
Utalii ni muhimu pia, kwa sababu karibu na Aswan kuna mabaki mengi ya mahekalu na majengo mengine ya enzi za Misri ya Kale.