Babu kwa mjukuu wake ni hasa baba wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%.
Inakadiriwa kwamba miaka 30,000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mang'amuzi mbalimbali kuliko awali.[1][2]
Pia babu anaweza kushika nafasi ya baba ikiwa huyo hayupo (k.mf. amekufa) na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama baba yupo, babu anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto.