Bahari Nyeupe ni bahari ya pembeni ya Bahari Aktiki upande wa kaskazini ya Urusi ya Kiulaya ikipakana na mikoa ya Murmansk Oblast, Karelia na Arhangelsk Oblast. Inazungukwa na nchi kavu pande tatu hivyo ni kama ghuba kubwa la Bahari ya Barents. Eneo lake ni la km² 90,800.
Bandari muhimu ni Arkhangelsk. Kupitia mito na mifereji kuna njia za maji hadi Bahari Baltiki na Bahari Nyeusi.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari Nyeupe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |