Baja California (jimbo)

Isla Partida,Baja California
Nembo ya Sonora
Mahali pa Baja California katika Mexiko

Baja California (tamka ba-kha ka-li-for-ni-a, kwa maana Kalifornia ya Chini) ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kaskazini-magharibi ya nchi. Jimbo lina wakazi wapatao 2,844,469 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 69,921.

Mji mkuu ni Mexicali na mji mkubwa ni Tijuana. Iko kwenye pwani la Pasifiki na Ghuba ya California (au Bahari ya Cortez).

Imepakana na Marekani (jimbo la Kalifornia), halafu majimbo ya Meksiko Sonora na Baja California Sur.

Gavana wa jimbo ni José Guadalupe Osuna Millán.

Lugha rasmi ni Kihispania.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne