Barabara

Baraste kuu huwa na njia zilizotengwa kwa kupunguza hatari ya ajali
Barabara nyingi katika Afrika bado hazina lami zikihitaji matengenezo za mara kwa mara hasa baada ya mvua
Barabara ya Roma ya Kale huko Pompei, Italia.

Barabara ni njia iliyotengenezwa ili kupitisha binadamu akitumia vyombo vya usafiri kama vile magari, pikipiki, baiskeli pamoja na farasi.

Lengo ni kurahisisha mawasiliano toka mahali hadi mahali, hivyo ni kati ya miundombinu muhimu zaidi.

Huko Misri barabara za kwanza zilitengenezwa miaka 2,200-2,600 iliyopita,[1] lakini ziliwahi kuwepo za miaka 4,000 KK huko Ur, Iraq.

  1. John Noble Wildord (1994-05-08). "World's Oldest Paved Road Found in Egypt". New York Times. Iliwekwa mnamo 2012-02-11.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne