Barak (kwa Kiebrania בָּרָק, Bārāq) mwana wa Abinoam alikuwa kiongozi wa jeshi la makabila ya kaskazini wakati wa Waamuzi wa Biblia.
Kadiri ya Waamuzi 4-5 alikomboa Israeli kutoka mikono ya Wakananayo akishirikiana na nabii Debora[1]. Ilikuwa mwaka 1125 KK hivi.
Waraka kwa Waebrania 11:32-34 unamsifu kwa imani yake iliyompa ushindi.
Waamuzi 12 na wengineo |
---|