Baudolino

Mt. Baudolino alivyochorwa amevaa kiaskofu, kinyume cha ukweli.

Baudolino (pia: Baudilio; Villa del Foro, Alessandria, 700 hivi – Villa del Foro, 740 hivi) alikuwa mkaapweke huko Italia Kaskazini [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Novemba[2].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91332
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne