Beki (kutoka neno la Kiingereza "back"; pia mlinzi kutoka kitenzi "kulinda") ni mchezaji wa nafasi ya ulinzi karibu na goli katika michezo mbalimbali kama vile: mpira wa miguu, ragbi, hoki ya ugani n.k.
Katika soka, beki ni mchezaji wa ndani ambaye jukumu lake la msingi ni kuzuia wachezaji wa timu pinzani wasifunge katika lango lao, akicheza mbele ya Golikipa.
Kuna aina nne ya mabeki: Beki wa kati, Mfagiaji, Beki wakabaji na Beki wasaidizi. Beki wa kati na Beki wakabaji ni nafasi ambazo ni muhimu katika mifumo mingi. Beki wasaidizi na wafagiaji hutegemea aina ya mfumo unaotumika.