Bendera ya Ethiopia

Bendera ya kitaifa ya Ethiopia
Bendera ya serikali ya mapinduzi ya DERG iliyotumika 1975 hadi 1996
Bendera ya Ufalme wa Ethiopia ionyeshayo Simba wa Yuda. Bado inapendwa na watu wanaosimama upande wa marehemu Haile Selassie na hasa waumini wa imani ya Rastafari

Bendera ya Ethiopia mara nyingi inatajwa kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika. Rangi zake ni kijani kibichi, njano na nyekundu. Kutokana na sifa za Ethiopia za kuwa nchi ya pekee katika Afrika iliyojitetea dhidi ya uvamizi wa ukoloni. Rangi zake zilikuwa kama alama ya umoja na uhuru wa Afrika zikatumika kama rangi za Umoja wa Afrika katika bendera za nchi nyingi za Kiafrika.

Bendera ya rangi tatu ilitumika Ethiopia tangu karne ya 19 BK. Wakati wa serikali ya kifalme ilikuwa na nembo ya simba ya Yuda. Serikali ya mapinduzi ya DERG ilifuta simba na kubadilishabadilisha nembo za katikati. Tangu 1996 bendera imekuwa na nyota ya pembetatu.

Kama sifa hiyo ya kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika ni kweli inategemea na namna ya kuangalia Afrika. Kwenye Afrika ya kijiografia jinsi inavyotajwa leo dola za Afrika ya Kaskazini ziliwahi bila shaka kutumia bendera tangu karne nyingi yaani muda mrefu kabla ya karne ya 19.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne