Bendera ya Ubelgiji ina milia mitatu ya wima ya rangi neyusi - dhahabu na nyekundu. Muundo wa wima umetokana na mfano wa bendera ya Ufaransa, rangi ni za kihistoria za utemi wa Brabant.
Rangi hizi za kihistoria zilikuwa muhimu wakati wa uasi wa Wabelgiji dhidi ya Uholanzi mwaka 1830.
Baada ya uhuru bendera hii ilianzishwa rasmi kama bendera ya kitaifa katika mwezi wa Januari 1831.