Benyamini I wa Aleksandria (Barshut, Misri, 590 - 16 Januari 662) kuanzia mwaka 623 hadi kifo chake alikuwa Patriarki wa Aleksandria (Misri) na Papa wa 38 wa Kanisa la Wakopti ambalo linamheshimu kama mtakatifu.
Ni kati ya mapatriarki wake bora, akiongoza katika kipindi kigumu cha Misri kutekwa na Waajemi, halafu na Wagiriki na hatimaye na Waarabu.