Bertino wa Sithieu (Konstanz, leo nchini Ujerumani, 615 - Therouanne, leo nchini Ufaransa, 698 hivi) alikuwa mmonaki wa Kanisa Katoliki, mwanafunzi wa Kolumbani.
Pamoja na Momelini alianzisha monasteri iliyovutia miito mingi akafanya umisionari mkubwa Kaskazini mwa Ufaransa[1] [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Septemba[3].