Betrandi wa Comminges (L'Isle-Jourdain, Ufaransa, 1050 hivi – Lugdunum Convenarum[1], Ufaransa, 1126) alikuwa kanoni na shemasi mkuu wa Toulouse, halafu kwa karibu miaka 50[2] askofu wa Lugdunum Convenarum, akifanya juu chini kufufua na kurekebisha jimbo hilo kama alivyoelekezwa na Papa Gregori VII [3]
Pamoja na hayo, aliinua hali ya mji wa kale na kujenga upya kabisa kanisa kuu, alipoanzisha monasteri ya wakanoni chini ya kanuni ya Agostino wa Hippo [4].
Papa Honori III alimtangaza mwenye heri mwaka 1220/1222, halafu Papa Klementi V alimfanya mtakatifu mwaka 1309.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Oktoba[5].