Bikira ni mwanamke yeyote asiyewahi kuingiliwa kijinsia na mwanamume. Kwa sababu hiyo kizinda kinacholinda tumbo la uzazi hakijaondolewa, bali kinabaki kama ushahidi wa hali hiyo.
Katika utamaduni wa makabila mbalimbali, kufikia ndoa katika hali hiyo ni jambo linalothibitisha msimamo wa mwanamwali unaotumainisha atakuwa mwaminifu kwa mume wake.
Kati ya wote waliokuwa na sifa hiyo, maarufu zaidi ni mama wa Yesu wa Nazareti ambaye kwa heshima anaitwa kwa kawaida Bikira Maria.
Kufuatana na mfano wake, Wakristo wengi kuanzia karne ya 1 waliamua kutunza hali hiyo maisha yao yote, hasa katika utawa.