Bill Buchanan

Bill Buchanan
muhusika wa 24

James Morrison kama Bill Buchanan
Imechezwa na James Morrison
Misimu
4, 5, 6, 7
Maelezo

Bill Buchanan ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika unachezwa na James Morrison. Humu kacheza kama Mkurugezi wa Kitengo cha Kuzuia Ugaidi cha Los Angeles (CTU), kuanzia msimu wa nne hadi wa sita, pale alipolazimishwa ajiuzuru.

Katikati ya Msimu wa 5 na 6, amemwoa Karen Hayes.[1] Amerudi tena katika msimu wa 7, anafanya kazi kama kachero wa kujitegemea juu ya kufichua njama za magaidi katika serikali kuu. Yeye, Tony Almeida, Michelle Dessler, David Palmer, na Mike Novick wamefanya mpango wa kuongopea kifo cha Jack Bauer ili asitiwe kizuizini na serikali ya nchi ya China kwa kosa la kuvamia ubalozi wa China kinyume cha sheria.

  1. Owen, Rob (15 Aprili 2007). "Supporting players get to shine". Pittsburgh Post-Gazette. Iliwekwa mnamo 2008-07-08.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne