Billboard

Billboard ni jarida la Kimarekani ambalo hutolewa kila wiki kwa ajili ya soko la muziki. Hii huhesabiwa mara kwa mara kama 'kitu adimu sana' katika masuala ya burudani, na chapisho rasmi la soko la muziki; na linahesabiwa kama moja ya jarida linaloelezea habari za muziki tu bila kuchanganya habari nyingine mbali na muziki. Inaelezea chati za rekodi za kimataifa na nyimbo na albamu maarufu katika uainisho mbalimbali kwa wiki. Miongoni mwa chati muhimu sana ni pamoja na Billboard Hot 100 inatathmini nyimbo 100 bora bila kutazama aina ya nyimbo na kuchukuliwa kama kipimop sanifu cha kutathmini nyimbo hizo kwa Marekani, wakati Billboard 200 inatupia macho kwenye matokeo ya mauzo ya albamu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne