Black Reign ni jina la kutaja albamu ya tatu ya msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani - Queen Latifah. Albamu ilitolewa mnamo tar. 16 Novemba 1993 huko nchini Marekani. Ukilinganisha na hujudi za albamu zake mbili za awali, Black Reign ilikuwa albamu yake yenye mafanikio makubwa kwa hadi muda huu kwa Latifah, kwa kushika nafasu ya sita katika chati za Billboard 200 na kwenda hadi katika nishani ya dhahabu kwa RIAA. Albamu pia ilishika nafasi ya kumi na tano katika chati za Top R&B/Hip-Hop Albums.
- ↑ Christgau, Robert (1994). "Consumer Guide Album". The Village Voice. Iliwekwa mnamo 2012-01-25.