Bonde la Kamalondo ni eneo lenye majimaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sehemu ya bonde hilo iko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Upemba, na linafanyizwa na Mto Lualaba.
Wakati mmoja, huenda eneo hilo lilikuwa na ziwa moja kubwa. Kwa sasa lina maziwa 50; makuu ni maziwa ya Upemba na Kisale.