Boniface Nyema Dalieh (9 Desemba 1933 – 25 Aprili 2014) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Liberia.
Alipata daraja ya upadre mwaka 1965 na aliteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Cape Palmas tarehe 17 Desemba 1973, na askofu wa Talaptula. Alipewa daraja ya uaskofu tarehe 17 Machi 1974 kwa mkono wa Askofu Mkuu Thomas Joseph Brosnahan, na askofu Francis Carroll na Anthony Saliu Sanusi walikuwa maaskofu wa kusaidiana. Tarehe 19 Desemba 1981, Vikariati hiyo ya Cape Palmas iliteuliwa kuwa Dayosisi ya Cape Palmas, na Askofu Dalieh kuwa askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo hadi alipopumzika tarehe 15 Oktoba 2008.[1]