Brazzaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo. Una wakazi 2,308,000 (mwaka 2019) ambao ni sawa na 40% ya wananchi wote.
Uko kando ya mto Kongo ukitazamana na mji wa Kinshasa ng'ambo ya mto.
Brazzaville una bandari kwenye mto Kongo na mwanzo wa reli kuelekea pwani.