Bruno wa Segni, O.S.B. (Solero, Italia Kaskazini, 1045 hivi – Segni, Italia ya Kati, 18 Julai 1123) alikuwa padri, mmonaki, halafu askofu wa Segni na kwa muda abati wa Montecassino.[1][2][3][2]
Alishirikiana na Papa Gregori VII na Mapapa wengine watatu katika kurekebisha Kanisa na kwa ajili hiyo aliteseka sana[4].
Hata maandishi yake ya kufafanulia Biblia yanaheshimiwa sana.
Tarehe 5 Septemba 1181 Papa Lucius III alimtangaza kuwa mtakatifu.[1]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Julai[5]
- ↑ 1.0 1.1 Saint Bruno of Segni. Saints SQPN (23 August 2017). Retrieved on 6 October 2017.
- ↑ 2.0 2.1 Salvador Miranda. Consistory celebrated in 1086 (I). The Cardinals of the Holy Roman Church. Retrieved on 6 October 2017.
- ↑ St. Bruno. New Advent. Retrieved on 6 October 2017.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/63375
- ↑ Martyrologium Romanum