Bwawa ni mkusanyiko wa maji mengi. Ni dogo kuliko ziwa na mara nyingi huwa limetengenezwa na binadamu. Kwa kawaida, maji huzuiwa kutumia lambo katika bonde la mto au katika ardhi iliyochimbwa, ili kuhifadhi maji. Ingawa kuna mabwawa yaliyo na neno 'ziwa' katika jina, tofauti kuu ni kuwa bwawa hutengenezwa na binadamu[1].