Cape Town Tigers ni klabu ya mpira wa kikapu nchini Afrika Kusini yenye makao yake jijini Cape Town.[1] Timu hiyo inapatikana katika kitongoji cha Gugulethu.[2] Ilianzishwa mwaka 2019, makocha ni Raphael Edwards na Vincent Ntunja. Mwaka 2021, klabu ilishinda ubingwa wa kitaifa Afrika Kusini ukiwa msimu wake wa kwanza katika mashindano hayo.